Thursday, July 14, 2011

ROSTAM AZIZ Ajivua Ubunge Na Ujumbe wa NEC ya CCM.

 


ROSTAM ametangaza uamuzi huo katika mkutano uliofanyika IGUNGA  Jumatano wiki hii  ambapo amesema hatua hiyo haitokani na kile alichokiita kuwa ni shinikizo ndani ya chama, bali ni dhamira yake binafsi ikiwa na lengo la kutoa fursa kwa watu wengine kushika nyadhifa hizo alizoziacha.
Alitangaza uamuzi huo katika mkutano  uliofanyika huko IGUNGA TABORA ambapo pamoja na mambo mengine alieleza historia yake katika uongozi ndani ya CCM ukiwemo ubunge wa jimbo la IGUNGA alioushika tangu mwaka 1995 huku akitaja mafanikio na changamoto alizokumbana nazo.
Baadhi ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo  walijaribu kumsihi  AZIZ abadili uamuzi wake, suala ambalo alilipinga na kuendelea kushikiria msimamo wake.
Hata hivyo ofisi za Bunge kupitia kwa Kaimu Katibu wake JOHN JOEL zimesema hazina taarifa.
Safari ya siasa ya ROSTAM AZIZ ndani ya bunge ilianzia mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa ambapo aliibuka mshindi katika jimbo la IGUNGA.
Mwaka 2000 vile vile alitetea kiti chake cha ubunge na mwaka jana alishiriki katika kinyang’anyiro na katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM, Dkt. JAKAYA KIKWETE, aliweza kunadiwa.
Ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ROSTAM aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho, mjumbe wa NEC na mweka hazina.
Mwishoni mwa kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya CCM kilichofanyika mjini DODOMA mwezi Aprili mwaka huu, Kamati Kuu ilijiuzulu na hivyo kutoa nafasi ya kuundwa kwa Kamati Kuu nyingine ambamo ROSTAM na wajumbe wengine kadhaa waliachwa
Mwanasiasa huyu pia ni mfanyabiashara ambapo kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika tovuti ya Bunge, Rostam ni Mkurugenzi katika kampuni za African Tanneries, Caspian construction, African Trade Development na katika kampuni ya Research on Business yeye ni Mkurugenzi Mtendaji.
Halikadhalika tovuti hiyo inaonyesha kuwa kielimu, ROSTAM ana shahada ya kwanza ya Uchumi
Mbunge wa IGUNGA kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ROSTAM AZIZ
Mbunge wa IGUNGA kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ROSTAM  AZIZ ametangaza kuachia nafasi za uongozi wa kisiasa alizokuwa akishikilia ukiwemo ubunge wa jimbo la IGUNGA mkoani TABORA ambao ameushikilia kwa takribani miaka 15  pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment