Thursday, July 14, 2011

Eritrean Red Sea FC footballers 'disappear' in Tanzania


Thirteen members of an Eritrean football team have failed to return home after a regional tournament in Tanzania, officials say.
After Red Sea FC lost the Cecafa championship semi-final on Saturday, only half of the team turned up for the return flight to Eritrea.
This is said to be the fourth time Eritrean footballers have disappeared.
Young Eritreans often try to escape poverty, a repressive government and national military service.
Tanzania Football Federation (TFF) Angetile Osiah told Reuters news agency that the matter had been reported to the law enforcement authorities to investigate.
"Some team members colluded in the incident by trying to stamp the passports of the missing players at airport immigration checkpoints but when a physical head count was conducted, it was discovered that 13 players were missing," he said.
Tanzania's Young Africans beat their rivals Simba 1-0 in Sunday's Cecafa final.

ROSTAM AZIZ Ajivua Ubunge Na Ujumbe wa NEC ya CCM.

 


ROSTAM ametangaza uamuzi huo katika mkutano uliofanyika IGUNGA  Jumatano wiki hii  ambapo amesema hatua hiyo haitokani na kile alichokiita kuwa ni shinikizo ndani ya chama, bali ni dhamira yake binafsi ikiwa na lengo la kutoa fursa kwa watu wengine kushika nyadhifa hizo alizoziacha.
Alitangaza uamuzi huo katika mkutano  uliofanyika huko IGUNGA TABORA ambapo pamoja na mambo mengine alieleza historia yake katika uongozi ndani ya CCM ukiwemo ubunge wa jimbo la IGUNGA alioushika tangu mwaka 1995 huku akitaja mafanikio na changamoto alizokumbana nazo.
Baadhi ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo  walijaribu kumsihi  AZIZ abadili uamuzi wake, suala ambalo alilipinga na kuendelea kushikiria msimamo wake.
Hata hivyo ofisi za Bunge kupitia kwa Kaimu Katibu wake JOHN JOEL zimesema hazina taarifa.
Safari ya siasa ya ROSTAM AZIZ ndani ya bunge ilianzia mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa ambapo aliibuka mshindi katika jimbo la IGUNGA.
Mwaka 2000 vile vile alitetea kiti chake cha ubunge na mwaka jana alishiriki katika kinyang’anyiro na katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM, Dkt. JAKAYA KIKWETE, aliweza kunadiwa.
Ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ROSTAM aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho, mjumbe wa NEC na mweka hazina.
Mwishoni mwa kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya CCM kilichofanyika mjini DODOMA mwezi Aprili mwaka huu, Kamati Kuu ilijiuzulu na hivyo kutoa nafasi ya kuundwa kwa Kamati Kuu nyingine ambamo ROSTAM na wajumbe wengine kadhaa waliachwa
Mwanasiasa huyu pia ni mfanyabiashara ambapo kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika tovuti ya Bunge, Rostam ni Mkurugenzi katika kampuni za African Tanneries, Caspian construction, African Trade Development na katika kampuni ya Research on Business yeye ni Mkurugenzi Mtendaji.
Halikadhalika tovuti hiyo inaonyesha kuwa kielimu, ROSTAM ana shahada ya kwanza ya Uchumi
Mbunge wa IGUNGA kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ROSTAM AZIZ
Mbunge wa IGUNGA kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ROSTAM  AZIZ ametangaza kuachia nafasi za uongozi wa kisiasa alizokuwa akishikilia ukiwemo ubunge wa jimbo la IGUNGA mkoani TABORA ambao ameushikilia kwa takribani miaka 15  pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Wednesday, July 13, 2011

EPIQ NATION YAFANA COCOBEACH


Jumapili, iliyopita kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel kupitia Bidhaa yake mpya ya EPIQ NATION iliandaa tamasha kabambe la muziki pale Coco beach kwa ajili ya vijana. 
Wasanii mbalimbali walikuwepo kutoa burudani ikiwemo Mwasiti, Diamond, Chidi Benz na Nameless Kutoka Kenya. Pia kulikuwa na ma underground kibao waliopewa fursa ya kuonyesha vipaji vyao vya kuimba, kuchana pamoja na kudansi Diamond akiwa jukwaani

Saturday, July 9, 2011

Afrika yapata taifa jipya la Sudan Kusini

sherehe Sudan Kusini
Jumamosi hii Julai 9 mwaka 2011 ni siku itakayoingia katika vitabu vya historia kote duniani baada ya machafuko ya takriban miongo miwili hatimaye moja ya nchi kubwa kabisa barani Afrika Sudan inagawanywa rasmi mapande mawili Kaskazini inayosalia kuwa Sudan na taifa jipya linalozaliwa Sudan Kusini. Umoja wa Mataifa , Jumuiya ya kimataifa , Wahisani, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na dunia nzima imeelekeza macho na masikio Juba mji mkuu wa taifa la 54 barani Afrika na Sudan yote kwa jumla , kuona historia ikiandikwa lakini kubwa zaidi nini kitakachofuata baada ya kujitawala.
Umoja wa Mataifa umejiandaa vilivyo kuhakikisha usalama umedumishwa ukizingatiwa kuna changamoto nyingi katika taifa hilo lililosambaratika na machafuko ambapo hadi sasa suala la Kordofan Kusini na Abyei yaliyoko mpakani yanatia mashaka. Kuchambua kwa kina histotia hii, matarajio na changamoto , mkuu wa idhaa hii Flora Nducha amezungumza na Dr Salim Ahmed Salim anayeifahamu vilivyo historia ya Sudan, aliyewai kuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Afrika na mpatanishi maalum wa Umoja wa Afrika katika mzozo wa Darfur.

Friday, July 8, 2011

Haye atakiwa marekani

Haye atakiwa Marekani
Friday, 08 July 2011 06:41
LOS ANGELES, Marekani

DAVID Haye, ameambiwa aende kupigana Marekani ili apate mafanikio kama bondia mwingine wa Uingereza, Amir Khan.Khan alikwenda kufanya mazoezi Marekani na akaja kuwa bingwa wa dunia baada ya kwenda Hollywood na kufanyishwa mazoezi na kocha mahiri wa Kimarekani, Freddie Roach.

Mtu maarufu katika ngumi, Richard Schaefer, anaamini kuwa kipaji cha Haye kinaweza kuzaliwa upya baada ya kupoteza pambano lake la uzito wa juu duniani kwa kupigwa kwa pointi dhidi ya Wladimir Klitschko, mjini Hamburg, Jumamosi usiku.

Haye sasa anataka kurudiana na Klitschko au kutwangana na kaka yake Vitali, ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC .

Lakini Schaeffer, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya promosheni ya Oscar De La Hoya, Golden Boy, ambaye ni promota wa Khan na Haye alisema, "anatakiwa kuja na kupigana mapambano Marekani kwa mara ya kwanza.

"David hakuweza kucheza vizuri Jumamosi na sikufurahishwa na uchezaji wake.

"Lakini si sahihi kumjaji David kwa uchezaji wa mechi moja. Ana umri wa miaka 30 na bado ni mzuri, ni mpiganaji anayefurahisha katika uzito.

"Hakuna anayejali kuhusu akina Klitschkos."

Wakati huohuo, Schaefer, amesema Khan anaweza kujiandaa kupigana kwa ajili ya kutwangana na Floyd  Mayweather mwakani.

Bingwa wa mkanda wa WBA, Khan, ameanza maandalizi ya kucheza pambano la kuunganisha mataji dhidi ya Zab Judah mjini Las Vegas, Julai 23.

Pambano lake linalofuatia linaweza kuwa dhidi ya Erik Morales, Desemba na kisha kurejea Uingereza ambapo bondia huyo mwenye miaka 24, atahamia katika uzani wa welter na anaweza kutwangana na Kell Brook.

Huenda akatwanga na  Mayweather Novemba 2012.

Schaefer alisema: "Hii ni mipango mikubwa kwa Khan.

"Nimekuwa na mazungumzo na Mayweather na yuko tayari kutwangana na Amir."
 
Haye atakiwa Marekani
Friday, 08 July 2011 06:41
LOS ANGELES, Marekani

DAVID Haye, ameambiwa aende kupigana Marekani ili apate mafanikio kama bondia mwingine wa Uingereza, Amir Khan.Khan alikwenda kufanya mazoezi Marekani na akaja kuwa bingwa wa dunia baada ya kwenda Hollywood na kufanyishwa mazoezi na kocha mahiri wa Kimarekani, Freddie Roach.

Mtu maarufu katika ngumi, Richard Schaefer, anaamini kuwa kipaji cha Haye kinaweza kuzaliwa upya baada ya kupoteza pambano lake la uzito wa juu duniani kwa kupigwa kwa pointi dhidi ya Wladimir Klitschko, mjini Hamburg, Jumamosi usiku.

Haye sasa anataka kurudiana na Klitschko au kutwangana na kaka yake Vitali, ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC .

Lakini Schaeffer, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya promosheni ya Oscar De La Hoya, Golden Boy, ambaye ni promota wa Khan na Haye alisema, "anatakiwa kuja na kupigana mapambano Marekani kwa mara ya kwanza.

"David hakuweza kucheza vizuri Jumamosi na sikufurahishwa na uchezaji wake.

"Lakini si sahihi kumjaji David kwa uchezaji wa mechi moja. Ana umri wa miaka 30 na bado ni mzuri, ni mpiganaji anayefurahisha katika uzito.

"Hakuna anayejali kuhusu akina Klitschkos."

Wakati huohuo, Schaefer, amesema Khan anaweza kujiandaa kupigana kwa ajili ya kutwangana na Floyd  Mayweather mwakani.

Bingwa wa mkanda wa WBA, Khan, ameanza maandalizi ya kucheza pambano la kuunganisha mataji dhidi ya Zab Judah mjini Las Vegas, Julai 23.

Pambano lake linalofuatia linaweza kuwa dhidi ya Erik Morales, Desemba na kisha kurejea Uingereza ambapo bondia huyo mwenye miaka 24, atahamia katika uzani wa welter na anaweza kutwangana na Kell Brook.

Huenda akatwanga na  Mayweather Novemba 2012.

Schaefer alisema: "Hii ni mipango mikubwa kwa Khan.

"Nimekuwa na mazungumzo na Mayweather na yuko tayari kutwangana na Amir."
 
DAVID Haye, ameambiwa aende kupigana Marekani ili apate mafanikio kama bondia mwingine wa Uingereza, Amir Khan.Khan alikwenda kufanya mazoezi Marekani na akaja kuwa bingwa wa dunia baada ya kwenda Hollywood na kufanyishwa mazoezi na kocha mahiri wa Kimarekani, Freddie Roach.

Mtu maarufu katika ngumi, Richard Schaefer, anaamini kuwa kipaji cha Haye kinaweza kuzaliwa upya baada ya kupoteza pambano lake la uzito wa juu duniani kwa kupigwa kwa pointi dhidi ya Wladimir Klitschko, mjini Hamburg, Jumamosi usiku.

Haye sasa anataka kurudiana na Klitschko au kutwangana na kaka yake Vitali, ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC .

Lakini Schaeffer, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya promosheni ya Oscar De La Hoya, Golden Boy, ambaye ni promota wa Khan na Haye alisema, "anatakiwa kuja na kupigana mapambano Marekani kwa mara ya kwanza.

"David hakuweza kucheza vizuri Jumamosi na sikufurahishwa na uchezaji wake.

"Lakini si sahihi kumjaji David kwa uchezaji wa mechi moja. Ana umri wa miaka 30 na bado ni mzuri, ni mpiganaji anayefurahisha katika uzito.

"Hakuna anayejali kuhusu akina Klitschkos."

Wakati huohuo, Schaefer, amesema Khan anaweza kujiandaa kupigana kwa ajili ya kutwangana na Floyd  Mayweather mwakani.

Bingwa wa mkanda wa WBA, Khan, ameanza maandalizi ya kucheza pambano la kuunganisha mataji dhidi ya Zab Judah mjini Las Vegas, Julai 23.

Pambano lake linalofuatia linaweza kuwa dhidi ya Erik Morales, Desemba na kisha kurejea Uingereza ambapo bondia huyo mwenye miaka 24, atahamia katika uzani wa welter na anaweza kutwangana na Kell Brook.

Huenda akatwanga na  Mayweather Novemba 2012.

Schaefer alisema: "Hii ni mipango mikubwa kwa Khan.

"Nimekuwa nazungumza na myweather na yuko tayari kutwangana na Amir

Thursday, July 7, 2011

CCM Kuanza Kusherehekea Miaka 50 Ya Uhuru

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mwaka huu Sehemu ya nchi yetu, yaani Tanzania Bara itaadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wake toka kwa Wakoloni. Uhuru huu uliopatikana miaka hamsini iliyopita ni kazi nzuri na ya Kizalendo iliyofanywa na Chama cha TANU.

Chama Cha Mapinduzi katika kukumbuka kazi hii nzuri ya kutafuta Uhuru wa nchi yetu kimeamua kufanya shughuli mbalimbali za kukumbuka kuzaliwa kwa chama kilicholeta Uhuru wa Tanzania Bara yaani TANU.

Itakumbukwa TANU ilizaliwa tarehe 7/7/1954 hapa Dar es salaam katika mtaa wa New street ambao kwa sasa unafahamika kama mtaa wa Lumumba mahali ambapo sasa ni  Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu. Huo ukawa ndio mwanzo wa harakati za kudai Uhuru, Utu na Heshima ya Mwafrika katika nchi yetu.

Kwa kuienzi historia na kazi nzuri na ya Kizalendo iliyofanywa na TANU, Chama Cha Mapinduzi kimeamua katika kuadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii zikiwa na kauli mbiu Uhuru na Kazi, kauli maarufu katika miaka ya nyuma ambayo Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere aliitoa katika hotuba yake ya kusisimua siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Mwalimu Nyerere aliitumia hotuba hiyo kuwaeleza wananchi wajiandae kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea wao wenyewe na nchi maenedeleo. Maadhimisho haya yatafanyika nchi nzima kuanzia ngazi za matawi na kuwashirikisha wanachama wetu na wananchi wote kwa ujumla. Shughuli zitakazofanyika ni kama zifuatavyo:-

     i.        Usiku wa kuamkia tarehe 7/7/2011 Vijana wa CCM nchini watakutana maeneo mbalimbali kufanya shamrashamra za kuzaliwa TANU

    ii.        Tarehe 7/7/2011 asubuhi wanachama wa CCM na wananchi watakutana kwenye matawi yao na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile, kufanya usafi, kusaidia ujenzi, kupanda miti, kutembelea wagonjwa mahospitalini n.k.

  iii.        Ikiwezekana kufanya matamasha mbali mbali yatakayowashirikisha vijana wasomi wanasiasa na wazee kujadili masuala mbali mbali yenye faida kwa Kata, Wilaya, Mkoa au Taifa kwa ujumla.

  iv.        Kufanya mikutano ya hadhara na kujikumbusha mafanikio yaliyopatikana kwa kila Mkoa na  Wilaya katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.

Kwa Sehemu kubwa tunategemea walezi wa CCM wa Mikoa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa watashiriki shughuli hizo mikoani. Sherehe hizi zitaanza usiku wa tarehe 6/7/2011 kwa vijana wa CCM sehemu mbalimbali nchini kukutana na kusherehekea ikiwa ni pamoja na kufyatua MAFATAKI saa sita usiku ya siku hiyo, kama ishara ya kuzaliwa TANU.

Mwenyekiti wa CCM Taifa Dr. Jakaya M. Kikwete atashiriki sherehe hizi mkoani Dar es salaam, usiku wa Tarehe 06/07/2011 na tarehe 07/07/2011 asubuhi atakutana na Mabalozi wa Nyumba Kumi Mkoa wa Dar es salaam.

Ni mategemeo yangu vyombo vya habari vitashirikiana nasi katika kuuelimisha umma kuhusu historia hii muhimu ya Taifa letu na kutangaza matukio yote yatakayo ambatana na maadhimisho haya.

Wednesday, July 6, 2011

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bunamwaya ya Uganda katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Kagame uliochezwa Julai 5,2011 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, sasa Simba imetangulia katika fainali hizo ambapo itamenyana na El Mereikh ya Sudan katika mechi ya nusu fainali mwishoni mwa wiki, ambapo El Mereikh ilikata tiketi hiyo baada kuifunga Ulinzi ya Kenya katika mchezo uliomalizika Julai 5,2011 kwa njia ya matuta

Saturday, July 2, 2011

Asema serikali imefanya maamuzi magumu



Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amejibu hoja zilizotolewa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, wiki iliyopita kuwa serikali ya awamu ya nne imeshindwa kufanya maamuzi magumu, kwa kuorodhesha mambo mbalimbali ambayo yamesema ni magumu yakiwa yamechukuliwa na serikali.

 Pinda alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana jioni.  Lowassa akichangia mjadala wa bajeti hiyo wiki iliyopita, alisema kuna ugonjwa wa kuogopa kutoa maamuzi hivyo akataka serikali kutoa maamuzi na kusema: 

 “Heri ukosee kwenye kutoa maamuzi kuliko kutotoa maamuzi. Toeni maamuzi, acheni kuogopa, tumepewa nchi, tufanyeni maamuzi. Heri uhukumiwe kwa kutoa mamuzi kuliko kwa kutotoa maamuzi. Toeni maamuzi. Nasema tunaweza kufanya. Tukinuia, tukiamua, tunaweza kufanya.”

 Pinda alisema serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Dk. Jakaya Kikwete ndiyo pekee imefanya maamuzi magumu na mazito kuliko serikali zote zilizopita.

 Alisema imekuwa ikifanya maamuzi thabiti na magumu, lakini kwa busara na tahadhari ili kutenda haki na kwa kuzingatia uwezo wake ili kulinda maslahi ya wananchi na kudumisha amani.

  Alisema katika kufanya maamuzi hayo, serikali imekuwa makini kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

 Aliyataja maamuzi magumu yaliyokwishafanywa na serikali ya awamu ya nne kuwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani waliokuwa mawaziri wa serikali zilizopita kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili za kutumia madaraka isivyo halali; na pia kujenga shule za sekondari za kata, ambazo zimewezesha wanafunzi wengi kupata elimu ya sekondari.

 Mengine ni kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom);  kujenga Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo; kukamilisha miradi yote 27 ya barabara kuu zilizoanzishwa na serikali ya awamu ya tatu; ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya maji nchini; na kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

 Pia, kuondoa mpasuko wa kisiasa Zanzibar na kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ); kupanua na kushamiri kwa demokrasia nchini kwa kiwango kikubwa; uhuru mkubwa wa vyombo vya habari; na kuruhusu kuanzisha mchakato wa kupata Katiba mpya. 

  “Lakini pia katika awamu hii ndipo tumefanya maamuzi mazito sana ya kuvunja Baraza la Mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Edward Lowassa. Hili nalo halikuwa jambo jepesi hata kidogo. Inataka Moyo!” alisema Pinda.

Aliongeza: “... maisha ya serikali katika kutekeleza majukumu yake kwa dhana ya uwajibikaji wa pamoja kupitia Baraza la Mawaziri. Tunachohitaji ni kuvumiliana. Kuvuta subira, kwani mambo mema hayataki haraka!  Tutaamua na Tutafanya!”
 Akizungumzia suala la posho, alisema suala hilo ni muhimu kutazamwa kwa upana wake na kwa msingi ulioelezwa chini ya Mpango wa Miaka Mitano, yaani kuzungumzia posho zote.  

“Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Waraka wa Masharti ya Kazi za Mbunge; stahili za wabunge ni pamoja na zifuatazo: Mshahara wa mbunge kodi Sh. 588,000 ambao ulishakatwa, ambao haujakatwa kodi  ni Sh. 2,305,000, ukisakatwa kodi ni Sh. 1,717,000. Posho ya ubunge; posho ya vikao vya Bunge na kamati zake,” alisema Pinda.

  Aliongeza: “Posho ya madaraka kwa viongozi; Entertainment Allowance (posho za maburudisho) kwa viongozi; posho ya kujikimu ndani na nje ya nchi; posho ya mavazi anaposafiri nje ya Tanzania; posho ya msaidizi wa ofisi ya mbunge; posho ya usafiri wakati wa vikao vya kamati na mikutano ya Bunge; vilevile, kuna posho ya mafuta (Lita 1,000) kwa mwezi na Mfuko wa Maendeleo wa Jimbo (CDCF).”

 Pinda alisema kwa kuwa suala hilo lipo ndani ya Mpango wa Maendeleo, serikali italitafakari kwa undani na kuangalia posho zipi hazina tija na zipi zina tija na manufaa ya kuongeza ufanisi ili ikiwezekana zihuishwe na kujumuishwa ndani ya mishahara au vinginevyo kama itakavyoonekana inafaa.

 Alisema serikali pia itaangalia suala la kupunguza gharama za matumizi ya serikali kwa ujumla wake ikijumuisha kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika taasisi zote za serikali.

  Pinda alisema kwa maelekezo ya Rais Kikwete, uamuzi wa kuhamia Dodoma hauna budi kutekelezwa na kusisitiza kuwa hata kama fedha zimetengwa, Ofisi ya Waziri Mkuu itajengwa Dodoma.

Friday, July 1, 2011

Tanzania kuanza kuchimba madini ya Urani

Duma
Duma wa Selou
Tanzania itaanza kuchimba madini ya urani katika mbuga ya wanyama ya Selous, eneo lililo chini ya udhamini wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughilikia mazingira maarufu kama World Heritage.
Akizungumza na Idd Seif wa Idhaa ya kiswahili ya BBC, Waziri wa maliasili na utali iwa Tanzania, Ezekiel Maige, alisema kuwa sehemu wanayohitaji kutumia kwa kuchimbia mgodi wa urani ni 0.69%,
hivyo kupunguza eneo la mbuga ya wanyama kwa chini ya 1%.
Kwa mujibu wa Waziri Maige, WHC imesema itatoa kibali iwapo tu masharti ya kutunza mazingira yatakuwa yamezingatiwa. Fedha zitakazopatikana kutokana na madini hayo zitasaidia kutunza
mbuga hiyo alisema Maige.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Utamaduni UNESCO, hekta milioni tano la hifadhi ya mbuga ya Selou ina idadi kubwa ya Tembo, vifaru weusi, Chita, viboko na mamba na haijaharibu na
shughuli zozote za kibinadamu.
Katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bw Maige alisema mradi huo bado uko katika hatua za mwanzo lakini utaathiri kwa asilimia 0.69 tu ya mbuga ya sasa na utakuwa ni chanzo muhimu
cha mapato ya nchi.
Makampuni yanatarajia kupata $200 milioni kwa mwaka kutokana na uchimbaji wa Urani na kati ya hizo $5 milioni zitalipwa kwa serikali ya Tanzania, alisema.
Sehemu ya mapato hayo itasaidia kutunza mbuga hiyo na mradi utatoa ajira kwa watanzania 1,600.
Katika mkutano wa mwaka wa kamati ya WHC, waziri Maige alisema, kulikuwa pia na wasiwasi kuhusu Msitu wa hifadhiwa Undendeule ulio kusini mwa mbuga ya Selou.
Lakini Bw Maige ambaye pia anashughulikia Utalii alisisitiza kuwa hakutakuwa na mathara kwenye msitu huo wa hifadhi ambao kwa sasa unaigharimu serikali $490,000 kwa mwaka kuutunza. Na
mapato yatakayotokana na uchimbaji wa madini hayo utasaidia kulipa askari wanaodhibiti ujangili.
Alisema Tanzania haikuhitaji kibali kutoka UNESCO ili kuendelea na mpango wake wa kuchimba Urani, lakini mataifa ya Afrika Mashariki yalitaka kujiridhisha na mapendekezo ya shirika hilo.
"mradi huu wa Urani utaanza," aliiambia BBC.
Aliongeza kuwa WHC Tanzania ifanye tathmini yenyewe itakayopitishwa na Tume ya Mazingira ya nchi hiyo.
Hatua ya pili ilikuwa ni hitaji la ujumbe wa wataalam kutoka UN kutembelea aeneo hilo na kutoa mapendekezo yake kuhusu kulinda na kutunza mfumo wa ekolojia.
Waziri alisema baada ya uamuzi huu taarifa itapelekwa katika mkutano mwingine wa WHC mwakani kuhusu mipaka ya Mbuga ya Hifadhi ya Selou.
Bw Maige aliongeza kuwa utafiti unaonyesha kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu sumu ya mionzi inayotokana na uchimbaji wa Urani katika eneo hilo.
"Kiwango cha mionzi kitabakia kuwa kile kile, haitakuwa na hatari kwa binadamu," alisema.

Strauss-Khan aachiwa bila dhamana

Aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF Dominique Strauss-Khan ameachiwa huru baada ya kupewa kifungo cha nyumbani na kurejeshewa dhamana yake ya dola za kimarekani milioni 3.7.
Imeripotiwa waendesha mashtaka wamekubaliana kuwa Bw Strauss-Khan aachiliwe huru "kwa udhamini wake mwenyewe," ikimaanisha aahidi kufika mahakamani.
Anatuhumiwa kumdhalilisha kijinsia mhudumu kwenye hoteli moja mjini New York mwezi Mei 14.
Bw Strauss-Khan na mkewe

Lakini kesi hiyo inakaribia kufutwa baada ya kuibuka mashaka makubwa juu ya uaminifu wa aliyemshtaki.
Mwanasiasa huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 62 - aliyeonekana kuwa miongoni mwa wagombea wa urais wanaoongoza- alifika mahakamani siku ya Ijumaa.
Baada ya kutathmini taarifa za mwendesha mashtaka kutoka kwenye ofisi ya mahakama ya wilaya ya Manhattan, jaji ametangua masharti makali ya dhamana aliyopewa na Bw Staruss-Khan, lakini aliamuru kushikiliwa kwa hati yake ya kusafiria ili asiweze kusafiri nje ya Marekani.
Miongoni mwa yaliyowasilishwa ni taarifa kuwa mhudumu huyo alitoa ushahidi usio wa kweli kwa wazee wa baraza, bila kusema alisafisha chumba chengine kabla ya kumwambia msimamizi wake juu ya madai ya kudhalilishwa kijinsia.

BARACK OBAMA NA MATUMAINI FEKI YA WAAFRIKA NA WEUSI

 
Mapema mwezi wa Juni, tarehe 3 mwaka huu, Barack Obama alifikia hatua kubwa katika harakati zake za kuteuliwa mgombea wa Chama cha Democratic. Ni hatua ambayo Wamarekani wanaiita (Nominee designate) mgombea mtarajiwa. Siku hiyo hapa Tanzania mkutano wa nane wa Taasisi ya Sullivan ulikuwa ukifanyika. Aliyewahi kujaribu harakati za kuchaguliwa, Mchungaji Jesse Jackson alinena kwa furaha akijivunia ni ushindi kwa weusi. Karibu waongeaji wote walizungumza juu ya hili kwa maono ya ushindi wa weusi.
Nikiwa kama mtanzania, mtu mweusi, nimefarijika pia kwa ushindi wa Seneta Barack Obama. Kufarijika kwangu si kwa mashiko ya rangi; yaani mweusi kashinda basi nami nifurahi. Kwangu nimeshangazwa karibu weusi wote wanamshabikia Obama eti kwa kuwa ni mweusi. Nina mashaka kama kweli hisia zetu zinaegemea zaidi rangi basi nadiriki kusema kuwa tusipokuwa makini nasi pia ni wabaguzi wa rangi wakubwa.
Nina wasiwasi: wote wanaouchukulia ushindi wa Obama kama ushindi kwasababu ni mweusi basi wamepotea njia. Ni lazima watu tufikiri kwa kina na si kushabikia tu ilihali inawezekana kabisa Obama hatakuwa na maslahi yoyote kwa waafrika na hata kwa watu weusi sehemu mbalimbali za dunia.

Labda niwarejeshe kwenye historia: Raisi wa zamani wa Marekani, Ruthirford Hayes aliwahi kunena kuwa “Us government is a government of the corporations, by corporations for the corporations”. Alimaanisha kuwa serikali ya Marekani ni serikali ya Makampuni, kwa maslahi ya Makampuni na inaendeshwa na Makampuni. Hapa alikuwa anajaribu kutanzua kiza kinene (illusion) kwenye maana ya demokrasia kama ilivyokuwa imeelezwa awali na mtangulizi wake Lincoln pale alipoweka maneno: “Government of the People for the People by the People” yaani: “serikali ya watu, kwa watu na maslahi yao” katika katiba ya nchi hiyo.

Ni katika msingi wa kuingalia serikali ya Marekani kama inayoongozwa na mtizamo wa Katiba kuheshimiwa bila ubazazi wa aina yeyote kama tunavyoshuhudia hapa kwetu, basi kama Obama atachaguliwa kuwa raisi wa Marekani tujue kabisa atafanya kazi kwa misingi ya Rais wa zamani Ruthirford Hayes. Hapa ndipo panaponifanya nisiwe na matumaini kama kweli mtu mweusi kuwa Rais wa Marekani basi tutafaidika na lolote tofauti na marasi wengine weupe waliokwishapita na kutawala Marekani. Ni vyema tumfurahie Seneta Obama kutokana na wajihi wake: ni jinsi gani ameweza kuchambua masuala mbalimbali kwa ufasaha na kuonesha jinsi gani anavyoweza kufikiri. Ni kigezo hiki tu naweza kufurahia ushindi wa Obama na wala kamwe si rangi yake. Kinyume na hapo naona ni mtizamo wa kibaguzi ambao hauna nafasi katika dunia ya kileo.

USHINDI HARAKATI ZA MTU MWEUSI

Kuna wengine wanauona ushindi wa Seneta Obama kama vile ni ushindi wa harakati za kutafuta haki za mtu mweusi. Hebu nikumbushie harakati za kumkomboa mtu mweusi nadhani zilianza siku nyingi chini ya watu kama akina Willium Du Bois, Marcus Garvey, George Padmore, Malcolm X, Martin Luther King, Nelson Mandela, Julius Nyerere, Jomo Kenyatta, Kenneth Kaunda, Robert Nesta Marley hadi akina Jesse Jackson na Luis Farhani wa leo hii Marekani.

Nimejaribu kupiga picha na nimeona hadi leo hii mtu mweusi kafikia mafanikio mengi katika nyanja nyingi. Kwa mfano, miongo mitatu iliyopita tunaweza kung’amua mafanikio ya mtu mweusi kama ifuatavyo:
Mosi, mwishoni mwa miaka ya 1970, waafrika weusi wa Marekani waliweza kutawala fani ya muziki kimataifa pale mziki aina ya kufokafoka ulikuwa sana kuanzia New York na kuua kabisa muziki wa Rock uliokuwa ukitawala.
Pili, baada ya mafanikio ya muziki, mwafrika asilia alianza kuonesha mafanikio duniani katika mchezo wa soka. Mwaka 1990, timu ya Taifa ya soka ya Cameroon (Indomitable Lions) ilifikia hatua ya robo fainali ya Kombe la dunia kule Italia chini ya Roger Milla. Baadaye mwaka 2002 kule Korea na Japan timu nyingine ya Senegal nayo ilifika hatua kama hiyo.

Jambo la tatu, katika miaka hiyo hiyo ya 1990, kule Afrika ya Kusini, Nelson Mandela na wafungwa wenzake kama akina Govan Mbeki, Walter Sisulu waliachiwa huru. Baadaye mwaka 1994 waafrika walio wengi wakafanikiwa kuunda serikali ndani ya nchi ambayo walinyimwa haki hiyo kwa miongo kadhaa. Si hapa Afrika tu mtu mweusi kafanikiwa, kwa mfano, mwaka 1997, kijana mweusi wa Marekani: Eldrick ‘Tiger’ Woods akaweka historia kushinda mashindano makubwa ya mchezo wa gofu “US Masters” na ametawala mchezo huo kidunia hadi ninapoandika makala hii. Mchezo wa kikapu ndio usiseme, mtu mweusi katawala hasa.

TIJA YA MAFANIKIO YA MTU MWEUSI

Kwa ujumla mtu mweusi kafanikiwa sana kwa miaka ishirini iliyopita si kwenye fani ya sanaa na michezo tu. Bali hata kwenye mambo ya uongozi wa taasisi nyeti za kimataifa, mwafrika tayari anajivunia kuweza kuongoza katika nyadhifa za juu kabisa. Kwa mfano, Umoja wa Mataifa (UN) , mwaka 1991 – 1994 ulikuwa chini ya Butros Butros Ghali raia wa Misri, baadaye akarithiwa na mweusi hasa Koffi Atta Annan wa Ghana mwaka 1995. Ni kipindi hichohicho, Jumuiya ya Madola ilikuwa chini ya Chief Emeka Anyaoku wa Nigeria kama Katibu Mkuu. Haya yote ilikuwa ni kuionesha dunia kuwa mtu mweusi anaweza na anatambulika. Lakini tujiulize: Je kulikuwa na msaada gani mkubwa kwa waafrika pale yote haya yalipojitokeza? Nakumbuka tulifurahi na kushangilia kutokana na hisia zenye mashiko ya rangi.

Watu wengine wanaweza kujiuliza labda mafanikio mengi ya mtu mweusi niliyoyaelezea hayakutokea Marekani bali hapa Afrika chini ya waafrika. Lakini kwa sasa yanatokea kule Marekani, ambalo ndilo Taifa linalotoa mwongozo wa dunia basi hatuna budi kuwa na matarajio. Na hii ndio hisia ninayoiona miongoni mwetu wengi kama “matumaini feki”. Kwangu siamini hivyo na kamwe sitaamini. Labda nikumbushie tu pale Raisi George Bush alipoingia madarakani na kumteua Collin Luther Powel kama mweusi wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, yaani cheo cha juu kabisa baada ya Raisi na Makamu wake Marekani. Raisi Bush alimteua baadaye mweusi mwingine Condoleza Rice katika nafasi hiyo ya juu kabisa hadi wakati naandaa makala hii.
Pia ni miaka si chini ya mitatu iliyopita, mwafrika mzaliwa wa Uganda John Sentamu alichaguliwa kuwa Askofu wa jimbo la York huko Uingereza. Hii ni nafasi ya pili kwa cheo ndani ya kanisa la Anglikana duniani. Katika haya yote yanayohusu ukombozi wa mwafrika ni mafanikio ambayo wanaharakati wanatumia mara nyingi neno la kiingereza “African Renaissance” yaani kuzaliwa upya kwa mwafrika.
Kwangu hili naliona pia kwa mtizamo huo kwani mwafrika ameweza kuondokana na kadhia za kibaguzi za zamani. Lakini tujiulize swali: Hivi mafanikio yote hayo yamesaidiaje weusi wa dunia hii? Tuache ukichaa, hebu angalia hata kule Afrika ya Kusini sasa mtu mweusi anapinga mweusi mwenzake kuishi nchini mwake. Umasikini wa mtu mweusi uliosababishwa na ufisadi wa wanaharakati wa zamani umetufikisha hapa tulipo. African Reinassance imepoteza mwelekeo huko Afrika Kusini kwa Madiba. Yote ni kwasababu mtu mweusi amekubali awe mtumishi na wakala wa mfumo wa kiutawala wa aina ya: “ corporate by corporation for the corporation”. Akina Raisi Mbeki na wapigania uhuru wenzake wamegeuka umma wa weusi na kuacha kuwatumikia na kuyatumikia makampuni.

Vivyo hivyo, nadhani hata Seneta Barack Obama atafuata mwelekeo huohuo kwa kuitumikia katiba ya Marekani ambayo imejaa lugha ya giza ikimaanisha mambo ambayo kimatendo ni kinyume na maneno. Yaani ikifuata mwelekeo wa Raisi Hayes badala ya ule sahihi wa Lincoln.
Ndio maana nilishangazwa sana mara baada ya Obama kuthibitisha kuwa ni mgombea mtarajiwa, hotuba yake ya kwanza mjini Washington ilikuwa ni mbele ya umati wa watu 7000 uliojumuisha “Kamati ya Mambo ya Waisraiel – Wamarekani ( Jewish American Israel Public Affairs Committee – AIPAC. Tujiulize ikiwa weusi wengi ndio waliompigia kura ilikuwaje aanze na shukrani kwa Wayahudi?

Dhahiri mwelekeo hapa wa dunia lazima tutumie bongo kufikiri na si kufuata hisia tu. Barack Obama hana njia nyingine ila ataungana na wale wengine niliowataja awali kama alama ya “African Reinassance” ambao wamemtangulia katika kuwatumikia wazungu. Kwani katika demokrasia ya leo, ule mtizamo wa Raisi Lincoln ndivyo sivyo. Mambo ya ‘Serikali ya watu, kwa watu na maslahi yao’ ni hadithi ya alinacha. Democrasia leo ni kutumikia makampuni makubwa yenye ushawishi. Haya ndiyo yenye kupenyeza rupia kusaidia kampeni za akina Seneta Obama ili wayatumikie pindi watakaposhinda. Ni kama vile hapa kwetu Tanzania vigogo fulani walivyojiundia vikampuni kwa mgongo wa EPA ili kupata fedha za kampeni. Obama yeye hakutumia mbinu za kibazazi za kujiundia vijikampuni feki ila anafadhiliwa na makampuni ambayo lazima alipe fadhila.

Mwisho, Seneta Obama ataungana na waliomtangulia: Koffi Annan, Colin Powel, Condoleza Rice, Chief Emeka Anyaoku na hata mama yetu mpendwa Asha Rose Migiro ambao walitumika na wengine wanatumika kwa sasa kama kielelezo feki cha kioo cha ubinadamu wa serikali za Marekani na Ulaya kukubalika ulimwenguni mbele ya umma wa watu weusi. Kwa mtizamo wangu huu ni lazima wale wote wenye mawazo kuwa Obama atasaidia weusi na hasa sisi waafrika waandike maumivu na masikitiko. Kwani akishakuwa Rais, kipaumbele kitakuwa ni maslahi ya Marekani kwanza kwa kufuata maneno ya Raisi Rutherford Hayes. Yaani kutumikia makampuni mbalimbali kabla ya kutumikia wapiga kura. Je tutarajie kama Raisi wa Marekani hatumikii watu wake, je atatumikia watu walio mbali naye kama sisi waafrika? Tuache ubaguzi tufikiri sana na tuangalie kwa bongo zetu na si kwa mioyo.

KUMBUKUMBU YA DKT MARTIN LUTHER KING JR NA TAFAKURI KUHUSU "I HAVE A DREAM" YA NYERERE (MAKALA KATKA GAZETI LA "MTANZANIA" LA LEO

Powered by Translate


Siku chache zilizopita Wamarekani waliadhimisha siku ya Dakta Martin Luther King Jr,mmoja wa wapigania haki za Waamerika Weusi.Historia inamkumbuka Dkt King (aliyezaliwa mwaka 1929 na kuuawa kwa risasi mwaka 1968)kama nguzo muhimu katika kupigania haki za Waamerika Weusi nchini humo.Pengine kilichomfanya wanaharakati huyo akubalike zaidi ni imani yake ya kudai haki kwa njia za amani.

Miaka mitano kabla ya kuuawa,mwaka 1963,Dkt King alitoa hotuba ambayo hadi leo imeendelea kuwa na mvuto mkubwa sio nchini Marekani pekee bali pia sehemu mbalimbali duniani katika mapambano ya kudai usawa.Katika hotuba hiyo iliyopewa jina “I Have a Dream” (“Nina Ndoto”,kwa tafsiri isiyo rasmi),Dkt King alieleza matamanio yake kuona Waamerika Weusi na Weupe wakiishi pamoja kwa amani na usawa.Hotuba hiyo iliyotolewa mbele ya watu zaidi ya laki mbili,inakubalika miongoni mwa wengi kama moja ya hotuba za muhimu kabisa katika historia ya Marekani.Mwaka 1999,hotuba hiyo ilichaguliwa na wasomi kuwa ni hotuba bora kabisa za karne ya 20.

Miongoni mwa nukuu muhimu katika hotuba hiyo ni pamoja na (kwa tafsiri yangu isiyo rasmi) “…nina ndoto kwamba siku moja taifa hili litasimama na kuishi kama inavyotamkwa kwenye imani yake….nina ndoto kwamba siku moja watoto wangu wanne wataishi katika taifa ambalo hawatahukumiwa kutokana na rangi ya ngozi zao bali tabia/utu wao….nina ndoto kwamba siku moja watoto wa waliokuwa watumwa na watoto wa waliokuwa wamiliki watumwa watakaa pamoja katika meza ya undugu…”

Msukumo uliotokana na uongozi wa harakati za Dkt King ulisaidia sana kubadili historia ya Marekani hususan usawa kwa (Wamarekani) Weusi, na kupelekea mabadiliko mbalimbali dhidi ya sheria za kibaguzi.Miongoni mwa sheria hizo ni pamoja na “Civil Rights Act” ya mwaka 1964 iliyoharamisha ubaguzi kwenye sehemu mbalimbali katika jamii.Mwaka uliofuata, “Voting Rights Act” ilipitishwa na kufuta kipengere kilicholazimisha wapiga kura watarajiwa kufanya testi za kupima uwezo wa kusoma na kuandika (wengi wa waathirika wa kipengere hicho walikuwa Wamarekani Weusi ambao walikuwa na maendeleo duni kielimu kutokana na kubaguliwa).

Maadhimisho ya siku ya Dkt King yamekuwa yakitoa changamoto nzuri kwa jamii ya Wamarekani kutafakari mahusiano kati ya Weupe na Weusi.Wengi hujiuliza iwapo ndoto za Dkt King zimetimia kweli,zinaelekea kutimia au hazina dalili ya kutimia kabisa.Ni maswali magumu ambayo yanahitaji uchambuzi wa kina kuyajibu,na pengine hata kwa uchambuzi wa kina bado inaweza kuwa vigumu kupata jawabu moja linalokubalika.Kingine kinacholeta ugumu wa kupata jawabu ni tofauti ya vizazi.Kwa walioishi nyakati za ubaguzi wa rangi na kushuhudia harakati za Dkt King wanaweza kuwa na mtizamo tofauti kuhusu kutimia kwa ndoto za mwanaharakati huyo ukilinganisha na kizazi cha hivi karibuni ambacho kinamwelewa Dkt King kupitia kumbukumbu za historia tu.

Hata hivyo ni rahisi kukubaliana kwamba harakati za Dkt King na wenzie zimesaidia kuleta mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na hayo ya kisheria niliyotaja awali.Wapo wanaokwenda mbali zaidi na kutoa mifano ya mafanikio ya Waamerika Weusi maarufu kama Jenerali Colin Powell na Condoleeza Rice ambao wameshika nafasi nyeti katika uongozi wa taifa hilo.Lakini mfano mzuri zaidi ni Barack Obama,seneta Mweusi anayewania kuteuliwa kugombea urais wa nchi hiyo kupitia chama cha Democrats.Akiteuliwa kuwa mgombea,ataweka historia ya pekee nchini humo,na akifanikiwa kushinda urais basi hiyo itakuwa zaidi ya kuweka historia (tuite kuandika historia upya).Hata kama atashindwa,mafaniko aliyokwishafikia hadi sasa ni hatua muhimu katika kutimia kwa ndoto za Dkt King.

Afrika nayo imetoa akina Dkt King kadhaa,na kwetu Tanzania tunajivunia Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere ambaye (kama Dkt King) alikuwa na ndoto zake kadhaa ambazo kimsingi zilihusu kuwa jamii yenye usawa.Ndoto za Mwalimu zilivuka mipaka ya Tanzania kuhakikisha kuwa Afrika yote inakuwa huru.Mchango wa Mwalimu katika mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika utaendelea kukumbukwa milele.Na pengine hapo ndipo baadhi yetu tunagundua mabadiliko ya vizazi yanavyochangia kusahaulisha historia.

Mara nyingi napokutana na vijana Waafrika wenzangu (wanaoishi hapa Uingereza) kutoka nchi kama Zimbabwe,Zambia,Angola,Msumbiji,Afrika Kusini,Namibia na Uganda,nabaini kwamba wengi wao aidha wamesahau au wanapuuza mchango wetu katika ukombozi wa nchi zao (kwa Uganda ni kumng’oa Nduli Idi Amini).Angalau Wazimbabwe wanaweza kuwa na kisingizio kwamba kutokana na ubabe wa Mugabe,baadhi yao wanaweza kutoona faida ya kumkimbiza mkoloni na kujipatia uhuru.

Lakini pengine si busara sana kuwalaumu wanaopuuza mchango wa Mwalimu na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa nchi zao kwani inawezekana kabisa wanafuatilia kinachoendelea nchini mwetu na kugundua kwamba baadhi yetu tumetupilia mbali kabisa jitihada za Baba wa Taifa kuhakikisha tunajenga jamii yenye usawa.Kwa vile dunia ni kama kijiji,katika zama hizi za utandawazi,majirani zetu hao watakuwa wanasoma na kusikia habari kuhusu ufisadi nchi mwetu,na pengine kubaki wanajiuliza “hivi hawa si ndio waliokuwa wanapigania usawa barani Afrika?Mbona wenyewe wako sasa wanafanyiana hivi?”.

Mwalimu alifariki huku baadhi ya ndoto zake zikiwa hazijatimia.Wachambuzi wazuri wa siasa wanadai kwamba baadhi ya ndoto hizo zilishindikana hata kabla hajang’atuka (kwa mfano upinzani wake wa awali dhidi ya ushirikiano na mashirika ya fedha ya kimataifa).Lakini nadhani Mwalimu aliumia zaidi kuona Azimio la Arusha likizikwa hai na Azimio “la kimyakimya” la Zanzibar (naliita hivyo kwani sijawahi kuona “document” yoyote rasmi inayoelezea kilichomo kwenye Azimio hilo).

Wakati Dkt King anaweza kufarijika huko aliko iwapo angeweza kufahamu baadhi ya mambo yanayoendelea sasa nchini Marekani (hususan kuhusu Obama) nashindwa kuhisi ni lipi litakalokuwa linampa furaha Mwalimu huko aliko tukiweka pembeni suala la amani na utulivu.Na hata katika hilo (la amani na utulivu) wapo wanaodai kuwa ni ya kufikirika zaidi kwani ni ukweli usiopingika kwamba masikini ni wengi zaidi kuliko matajiri,na yayumkinika kusema kwamba matumbo ya masikini hao hayana amani wala utulivu.

Kadhalika,kuna wanaodai kwamba kigezo cha amani na utulivu kimekuwa kikitumiwa vizuri zaidi na mafisadi wanaoamini kwamba Watanzania ni wapole sana na hawako tayari kuchezea lulu ya amani na utulivu kwa vile tu flani kakwiba mabilioni ya umma.Pengine mafisadi hao wako sahihi kwani tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu wakiua,wakapewa dhamana za chapchap na kuendela na maisha yao kama kawaida huku hatima ya kesi zao ikisubiri isahaulike akilini mwa watu.Wakati hayo yakitokea,magereza yetu yamejaa wamachinga wanaotafuta ridhiki mitaani na wafungwa wengine ambao inawezekana kabisa walijiingiza kwenye wizi wa nyanya au kuku kwa vile tu hawakuwa na njia nyingine ya kujipatia kipato.Uhalifu ni uhalifu,na kila mhalifu anastahili adhabu lakini inatatiza kuona wahalifu wengine wakiendelea kula raha kana kwamba waliyofanya si kinyume cha sheria.

Tofauti kubwa kati ya ndoto ya Dkt King na Mwalimu ni kwamba wakati Wamarekani Weusi wanafanya kila jitihada kuenzi jitihada za Dkt King kwa kuendeleza mapambano dhidi ya ubaguzi na kupigania usawa,sie tuko kwenye mgawanyiko mkubwa kati ya wachache walionacho wasiosubiri kuongezewa bali wanapora, na wengi wasio nacho ambao hata kile kidogo walicho nacho kinaporwa.Hili ndio tishio kubwa,sio tu kwa ndoto za Mwalimu,bali hata kwa hiyo lulu yetu ya amani na utulivu.