Thursday, June 30, 2011

TUZUNGUMZE MAPENZI!

 

Kila mtu anajua habari za mapenzi,hata wewe unayesoma habari hii unajua habari hizi. Mapenzi ni matunda matamu na pia ni matunda machungu.Sijui inategemea nini lakini nadhani ni kadri unavyoyapata,unavyoyala,na unavyojisikia wakati unaanza kula au unapomaliza.
Blog hii ni ya watu wazima,watu wanaojua nini maana ya mapenzi au wanaojaribu kujua zaidi.Nimeamua kuanzisha blogu hii kwa sababu najua ipo haja ya watu kuendelea kubadilishana mawazo juu ya mapenzi,ngono na mengineyo yanayohusiana na miili yetu,zikiwemo afya zetu.Si mnajua kwamba kitumbua siku hizi kimeingia mchanga ndugu zangu?

Kwa hiyo keti kitako tuanze kuyachambua masuala ya mapenzi. Kwa utaalamu wangu wa masuala haya nadhani nitakuwa tayari kujibu maswali yenu,hoja zenu nk kuhusiana na mapenzi,kujamiiana(ngono) na mengi mengineyo. Jisikie huru kunitumia email au kuuliza swali lako hapa hapa,nitakujibu. Lakini kwa kuanzisha hoja,hebu niambie,mapenzi ni nini kwa jinsi unavyoelewa wewe?Ni kwanini eti watu wanauana,wanafarakana,wanachinjana,nchi zinaingia kwenye vita kisa mapenzi? Je hayo yanabakia kuwa mapenzi au chuki? Kuna uhusiano gani kati ya mapenzi na wivu?Yupi ana nguvu kumshinda mwenzake?

WANAWAKE NA PESA


Msomaji mmoja wa blog hii kuhusu mapenzi (hakupenda kuweka jina lake) amekuwa wa kwanza kuuliza swali.Nitaliweka swali lake kwa kutumia italics likifuatiwa na jibu langu. Nitakuwa najaribu kuyaweka majibu yangu kwa ufupi sana(not in details) ili kuokoa nafasi na pia muda wako. Hata hivyo,tunaweza kuwasiliana kwa email kama utahitaji details zaidi na pia michango,mawazo,maoni nk yanakaribishwa sehemu ya mbele ya maoni.

SWALI:Sasa mimi nauliza kwa nini wasichana wengi wanapenda wanaume wenye pesa hata kama wana uwezo wa kupata pesa pia.Kwa nini wasijiamini nao kama wanaume na kufikiria kuwa pesa siyo jambo la maana sana kama unampenda mwenzio?

JIBU:Swali hili lina historia ndefu sana na ya aina yake. Ni swali lenye umri mkubwa pengine kama ilivyo dunia yetu. Ni swali zuri sana. Mara nyingi limeulizwa kwamba hivi mwanamke anataka nini zaidi,pesa,ulinzi au mapenzi na mapenzi motomoto kitandani?(Wenzetu wazungu lugha yao inaweza kutenganisha dhana hizi mbili kirahisi zaidi;love or good sex) Kwa bahati mbaya hata wanawake wenyewe wamejikuta kila mara wakipambanua mambo yote haya kwa sababu kwanza wanaume wenye sifa zote hizo hapo juu kwa pamoja ni kama hawapo na dunia imebadilika na inaendelea kubadilika.

Kabla sijaendelea mbele naomba ieleweke kwamba sio kila mwanamke anaweka pesa mbele na sio kila mwanamke duniani bado anaamini kwamb a yeye ni mtu wa kupokea,kuhudumiwa na kutunzwa tu.. Hali ni tofauti baina ya sehemu na sehemu,nchi na nchi,bara na bara,tamaduni na tamaduni. Kwa mfano hapa ninapoishi tamaa ya wanawake kupenda na kuthamini pesa inazidi kupungua kadri siku zinavyokwenda. Siku hizi wanawake nao wapo mstari wa mbele kuchangia kwa njia zote zinazowezekana kuboresha maisha na kwa maana hii mapenzi.

Sifa zinaenda kwa wale wanawake wanaojulikana kama “feminists” ambao kwa namna moja au nyingine wanachojaribu kufanya ni kumkomboa mwanamke kutoka kwenye fikra za yeye kuwa chombo cha kupokea tu bila kushiriki kwenye kutafuta na kutoa.

Pamoja na juhudi za dhati za wanasaikolojia katika kubadili muelekeo wa fikra za wale wanawake wanaothamini pesa na kubakia wakidhani kwamba jukumu la kutoa pesa,kuchangia matumizi,kuthamini mapenzi zaidi haliwahusu,bado wapo wengi wenye msimamo tofauti.Wao bado wamegubikwa na utando wa historia,utando wa saikolojia na pia utando wa nafasi ya mwanaume dhidi ya mwanamke au dhidi ya jamii inayomzunguka.

Msimamo wao ndio muuliza swali wetu, anaouwekea msisitizo;kwamba kwanini hata wale walio na hali nzuri kifedha bado wanadhani sio jukumu lao kusaidia,kuchangia katika matumizi?

Sababu kubwa,kama nilivyoanza kuanisha hapo juu ni fikra. Kihistoria,tangu mwanzo wa dunia hii mwanaume amekuwa mtafutaji na mwanamke akabakia nyumbani kulea watoto,kutunza kaya na kuhakikisha kwamba familia inakuwa bora. Katika nchi zetu za kiafrika,kwa mfano,utaratibu ukawa binti akue,akishavunja ungo basi aoelewe akaanzishe familia yake.Wazo la yeye kuandaliwa kama mtafutaji halikuwepo kabisa. Kwa bahati mbaya dunia tunayoishi hivi leo inatoa nafasi kidogo sana kwa ustawi wa taratibu kama hizo.Lakini je,fikra au utaratibu huo umetokomea vichwani mwa watu,hususani wanawake wenyewe? Jibu rahisi ni kwamba bado fikra ile ya mapokeo ipo miongoni mwa wanawake wengi.

Sababu ya pili ni ya asili kimaumbile na kisaikolojia vile vile. Kimaumbile mwanaume ameumbwa awe mkakamavu zaidi,awe mlinzi wa mwanamke.Ingawa siku hizi mambo yanazidi kubadilika ambapo utaona wanawake wengi katika shughuli ambazo hapo zamani zilidhaniwa kuwa za wanaume peke yao,bado kwa kiwango kikubwa, hali imebakia kama ilivyokuwa enzi za Adam na Hawa. Sasa “protection” hii haishii kwenye ulinzi wa kimaumbile tu kwamba nyumba ikivamiwa mwanaume ndiye anategemewa zaidi kuongoza mapambano dhidi ya wavamizi,bali huenda pia hata kwenye financial protectionism ambapo bila kujali mwanaume ana kiasi gani cha fedha,bado anategemewa kuwa mtoaji.

Mwishoni nashauri pia tusisahau watu wanaoitwa “sugar mummies”. Hawa pia ni wanawake ambao msimamo wao ni tofauti kabisa na wanawake wengi ingawa motives zao ni tofauti na mara nyingi zinaeleweka.Pengine siku moja tutapata nafasi ya kuzungumzia saikolojia zao pia.

KIDOKEZO: Hivi unafahamu kwamba mfalme wa Morocco wa karne ya 16 (Moulay Ismail) alikuwa na watoto wanaokadiria kufikia 1,042?

Zikowapi Tafiti za Muziki wa Kizazi Kipya - Fid Q



Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika miondoko ya Hiphop,Fareed Kubanda aka Fid Q ametoa wito kwa wadau wa sanaa hasa waandishi kujikita katika kuandaa machapisho na vitabu vinavyoelezea undani wa muziki huo.

Wito huo umekuja wakati ambao hakuna tafiti zinazofanywa katika muziki huo hapa nchini kiasi cha kutokuwepo kwa historia ya moja kwa moja inayoeleza asili ya muziki huo na nini hasa kilitokea hadi vijana wengi kujikita katika muziki huo ambao kwa sasa umepata umaarufu mkubwa.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii,Fid Q alisema kwamba,kumekuwa na ongezeko la watu kutoka nje wanaokuja kufanya utafiti kwenye muziki huu na kuondoka nao lakini waandishi na wadau wa sanaa wa ndani wamelala katika hilo na hawajaona fursa hiyo.

“Muziki huu una historia kubwa hapa nchini,watu wengi wanakuja kufanya utafiti,kuandika vitabu na kujizolea fedha.Hapa kwetu waandishi hawajaona haja ya kufanya hivyo.Wanaandika mambo madogo binafsi na kutojikita kwneye undani wa muziki huu”alilalamika Fid Q.

Aliongeza kwamba,kama juhudi za makusudi hazitaelekezwa katika kufanya tafiti na kutunza kumbukumbu za kutosha katika eneo hili,basi vizazi vitakosa kitu adhimu cha kukumbuka na kurithi.

“Tuna makundi mengi yalikuwepo kama Kwanza Unit na baadaye Hard Brastarz.Yalifanya kazi kubwa kusimamisha muziki huu hasa Hiphop nani anakumbuka? Tunahitaji kuweka mambo haya katika maandishi.Ni ajabu kukosa maandiko na tafiti katika mambo haya” alisisitiza

Kwa upande wake muasisi wa muziki huu na mwanzilishi wa moja ya makundi ya mwanzo katika muziki wa kizazi kipya la Kwanza Unit, Zavala alisema kwamba,wageni ndiyo wamekuwa wakihangaika na tafiti katika muziki huu lakini kwa waandishi wa nyumbani bado.

“Watu wanachota mamilioni katika kuandika miradi na tafiti kwenye muziki huu.Inashangaza hakuna waandishi waliokwisha kujitokeza kuandika vitabu na kufanya tafiti katika eneo hili linalovuta maelfu ya vijana” alilalamika Zavala.

Akihitimisha mjadala Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba,ni vema waandishi na wasanii wakajikita katika eneo la muziki wa kizazi kipya kwani hakuna machapisho na vitabu vya kutosha.

Shambulio la 11 Septemba 2001


Shambulio la 11 Septemba, 2001 ni tarehe na mwaka uliotokea mashambulio manne ya pamoja yaliyofanywa na kikosi cha Kigaidi cha al-Qaida dhidi ya Marekani. Kwa mujibu wa taarifa za maofisa, yasemekana kwamba kikosi cha Al-Qaida waliziteka nyala ndege nne wakazitumia kama silaha wakigongesha ndege katika majengo mjini New York na Washington DC kwa makusudi. Karibuni watu 3,000 walipoteza maisha katika shambulio hilo.

 Ndege zilitumika kufanyia Ughaini huo

Mabaki ya Jengo la WTC.
1. American Airlines Flight 11, iliyotumiwa kugonga mnara wa Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la mjini New York mnamo saa 8:46:30 asubuhi.
2. United Airlines Flight 175, ilitumiwa kugonga mnara wa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la Kusini mnamo saa 9:02:59 asubuhi. Watu wengi waliona tukio la pili kwasababu habari zilikuwa tayari zishasambaa katika mji na kila kamera za televisheni zilikuwa zikielekezea macho yao huko katika eneo la tukio, na wakati huo huo ndege ya pili ikagonga tena mnara wa Kusini mwa Jengo hilo.
3. American Airlines Flight 77, ilitumiwa kugonga jengo la Pentagon la mjini Arlington, Virginia (karibu kidogo na Washington DC), mnamo saa 9:37:46 asubuhi.
4. United Airlines Flight 93, hii haikubahatika kugonga mahala popote pale, badala yake wakaiangusha chini mnamo saa 10:03:11 asubuhi. Yaaminika ya kwamba magaidi hao walikuwa wakitaka kuigonga ndege hiyo katika jengo la mji mkuu wa Marekani. Abiria walijaribu kuinyang'anya Ndege hiyo kutoka mikononi mwa magaidi hao lakini hawakufanikiwa. Na matokeo Ndege ikashia kuanguka karibu na mji wa Shanksville, Pennsylvania.

 Matokeo ya maafa hayo

Jumla ya watu waliokufa katika shambulio hilo ni 246. Magaidi 19 waliuawa wakati wa shambulio hilo. Minara yote miwili ya jengo la World Trade Center yalipamba moto baada ya shambulio. Mnara wa Kusini (yaani WTC 2) liliungua kwa muda wa dakika 56 kbla ya kuanguka na kuangamia kabisa.
Jengo la Kaskazini (WTC 1) liliungua kwa muda wa dakikar 102 nalo pia lilianguka. Kama jengo la WTC lilivyoanguka, sehemu na mmong'onyoko wa jengo hilo lilipelekea majengo mengine yaliyoyazunguka majengo hayo kushika moto na kuharibika pia. Kutokaa na uharibifu uliotokea, jengo la tatu la 7 World Trade Center (7 WTC), nalo likaanguka mnamo saa 5:20 jioni. Baadahi ya mamjengo mengine yaliharibiwa vibaya na hata kuangamia kabisa yaani.
Takriban watu watu 2,602 walipoteza maisha katika Jengo la World Trade Center.
Ndege iliyogonga Pentagon iligonga chini mwa upande wa Magharibi mwa jengo hilo. Kisha ikagonga mpaka katika nguzo tano zinazoshikiria jengo hilo la Pentagon. Shambulio hilo Pentagon liliuwa watu 125.
Watu 2,973 walikufa katika shambulio hilo, wakiwemo watu watu wa zima moto waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya baadhi ya watu waliopatwa na balaa hilo.
Hili lilikuwa ndio shambulio kubwa la kwanza kwa watu ambao wasio Waamerika kushambulia nchini humo tangu mnamo mwaka wa 1941, pale Wajapani waliposhambulia kituo cha jeshi la maji kilichopo katika Bandari ya Pearl, Hawaii. Dhana nyingi zilikuwa zikionekana kwamba kuna watu katika Marekani walikuwa wakijua kwamba kutatokea na tukio kama hilo kabla na ni lini itakuwa hivyo.

 Vita dhidi ya ugaidi

Baada ya shambulio, Wamarekani wakawa wanawalaumu Al-Qaeda kwa kitendo walicho kifanya. Tangu hapo wakaianza vita dhidi ya Ugaidi. Kiongozi wa al-Qaeda, Osama bin Laden, Alikimbilia nchini Afghanistan. Serikali ya Marekani iliwaambia Serikali ya Afghanistan, iitwayo Taliban, kumsalimisha bin Laden mikononi mwao. Wataliban hawakufanya hivyo. Kiongozi wa Wataliban, Mullah Muhammad Omar, aliitaka Serikali ya Marekani impe Uthibitisho unaonyesha kwamba Osama anahusika na tukio hilo. Rais wa Marekani bwana George W. Bush akasema kwamba hakuna haja kutaka Uthibitsho wowote ule na Serikali ya Marekani ikaanzisha vita dhidi ya Afghanistan.

Wednesday, June 29, 2011

Historia ya GaddafiKanali Muammar Gaddafi ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na katika nchi za Kiarabu.

Gaddafi
Gaddafi

Ameongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 27.
Maarufu kwa nguo anazopenda kuvaa, na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am na hapo Umoja wa Mataifa ukaondoa vikwazo dhidi ya Libya.
Gaddafi mwaka 1969
Gaddafi mwaka 1969

Baada ya miezi kadhaa, serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za magharibi.
Hapo ndipo mabadiliko halisi yalionekana kwa kuwa nchi hizo za magharibi zilibadili mtazamo wao na kuacha kumtenga Gaddafi na kushirikiana naye hata kama alikuwa hatabiriki.
Ni mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake, kwa mujibu wa Saas Djebbar mtaalam wa siasa za Libya.
'Lakini ni mwanasiasa mashuhuri; hakuna shaka lolote kuhusu hilo. Ni mwanasiasa anayeweza kuhimili misukosuko ya kisiasa kwa hali ya juu sana.'

Asili ya Mabedui

Muammar Gaddafi alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942.
Gaddafi katika mkutano Sirte
Gaddafi katika mkutano Sirte

Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri na, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.
Gaddafi alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya, mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa 1969.
Ghaddafi alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Gaddafi alipokuwa akizuru Senegal mwaka 1985
Gaddafi alipokuwa akizuru Senegal mwaka 1985

Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Hema ya Gaddafi
Hema ya Gaddafi

Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.

Upekepeke

Benjamin Barber, mtaalam wa kisiasa wa kujitegemea, kutoka Marekani amewahi kukutana na Gaddafi mara kadhaa hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa Libya.
Gaddafi akiwa na viongozi wengine wa nchi za Uarabuni
Gaddafi akiwa na viongozi wengine wa nchi za Uarabuni

Bw Barber alisema kuwa Muammar Gaddafi anajihisi kuwa msomi aliyebobea.
Muammar Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 29 Mei 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.
"Utashangazwa kuwa ingawaje ni dikteta, ni mwanafalasafa na mwenye kutafakari jambo kabla ya kuzungumza," aliiambia BBC.
"Namchukulia sana kama mtu kutoka kabila la Waberber na mtu ambaye aliibuka kutoka tamaduni za watu wa jangwani, kutoka kwenye mchanga na kwa namna fulani kuna tofauti kubwa na uongozi wa kisasa, na kwa namna fulani hilo limemfanay awe mstahamilivu na mwenye msimamo."
Kanali Gaddafi amejitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou, kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.
Hivi karibuni aliongoza jitihada za kuwapatanisha waasi wa Tuareg kutoka nchi za Niger na Mali.

'Mbwa kichaa'

Jumuiya ya wanadiplomasia kuitenga Libya kulitokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation Organisation.
Gaddafi akiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Gaddafi akiwa na mwandishi wa habari wa BBC

Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.
Ilisemekana kuwa Kanali Gaddafi alitikiswa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.
Muuguzi wa Gaddafi
Muuguzi wa Gaddafi

Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano kati ya Washington na Libya.
'Hakutakuwa na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi' Kanali Gaddafi alisema alipokuwa akiiherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.

Changamoto za ndani


Kiongozi huyo wa Libya hujiona kama kiongozi wa kidini wa taifa hilo, akihakikisha kwa kile anachosema ni demokrasia.
Waandamanaji wa hivi karibuni Libya
Waandamanaji wa hivi karibuni Libya

Lakini katika hali halisi, wakosoaji wanasema Kanali Gaddafi amefanikiwa kudhibiti nchi hiyo.
Wanaompinga wamekandamizwa kikatili na vyombo vya habari vinabaki katika udhibiti mkubwa wa serikali.
Libya ina sheria ambazo haziwaruhusi watu kukusanyika katika misingi ya kisiasa zinazopinga mapinduzi ya Kanali Gaddafi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema serikali hiyo imewatia mbaroni mamia ya raia kwa kukiuka sheria hiyo na baadhi yao kuhukumiwa kifo.
Imeripotiwa kumekuwa na matukio ya utesaji na hata watu kupotea
Inadhaniwa kuwa Kanali Gaddafi anaandaa namna ya kukabidhi madaraka yake kwasababu ya umri aliyofikia sasa lakini haijulikani ni nani atakayerithi uongozi wa Libya kutoka kwa Gaddafi.
Sayf akiwa na ndugu yake Saad
Sayf akiwa na ndugu yake Saad

Kuna hisia kuwa mwanawe Sayf Al-Islam Gaddafi ndiye atarithi uongozi kutoka kwa baba yake na anaongoza katika kuleta mabadiliko.
Ingawaje Sayf ametangaza kuwa anastaafu siasa lakini kuna wanaohisi kuwa hii ni mbinu ya kuongeza ushawishi wake kisiasa.
Wakati huo huo, Gaddafi ameahidi kuwa wizara za nchi hiyo zitafutwa pamoja na bajeti zao
Utajiri utakaopatikana kutokana na mafuta utakabidhiwa moja kwa moja kwa wananchi.
Licha ya uchumi wa Libya kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje, mabadiliko bado yanakwenda taratibu.
Waandamanaji wakichana picha ya Gaddafi
Waandamanaji wakichana picha ya Gaddafi

Walibya wengi wana wasiwasi juu ya mabadiliko yanayotokea na kuhisi kuwa hawapati manufaa kutoka rasilmali ya Libya, waangalizi wanasema kwani huduma za serikali ni duni pamoja na ubadhirifu mkubwa wa mali.
' Wanajihadhari sana katika mapambano hayo kwa kuwa hawataki mabadiliko yatakayolegeza nguvu za umma,' alisema Saad Djebbar
'Lakini wakati huo huo, Walibya wanafahamu kuwa wanahitaji kufanya mabadilko. Na ndio maana wanaenda taratibu sana.
Mfuasi wa Gaddafi
Mfuasi wa Gaddafi

Wasifu: Osama bin Laden

Siku ambayo ndege zilizotekwa nyara ziligonga majengo ya World Trade Centre na makao ya wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ni vitendo vilivyombadilisha Osama bin Laden kutoka mtu mdogo asiyejulikana na kumfanya kuwa mojawapo watu wanaotambulikana sana duniani.
Osama bin Laden, katika mojawapo ya picha enzi za uhai wake.

Lakini alipojaribu kuepuka juhudi za Marekani kumkamata aliendelea kuwa kitendawili. Mawasilianao yake na dunia yalikuwa zaidi kwa kanda za video kupitia kituo cha televisheni cha Al Jazeera.
Bofya SIKILIZA WASIFU WAKE
Bin Laden aliwahi kunukuliwa akisema: "Kile ambacho Marekani inakionja hivi leo ni kitu kidogo sana ikilinganishwa na kile ambacho tumekuwa tukikipata katika miongo kadhaa. Taifa letu limekabiliwa na hali hii ya kudhalilishwa na kudharaualiwa kwa zaidi ya miaka 80. Wanawe wanauwawa, damu yao inamwagwa, maeneo yake matakatifu yanahujumiwa na hayatawaliwi kwa mujibu wa amri zake Mwenyezi Mungu."
Osama bin Laden alizaliwa mwaka 1957 katika familia yenye utajiri mkubwa. Baba yake alianzisha kampuni kubwa ya ujenzi katika Saudi Arabia. Akiwa ni miongoni mwa ndugu 18 wa kiume, Osama aliwahi kufanya kazi katika biashara hiyo ya familia. Maisha yake yalianza kubadilika alipokuwa kijana pale Muungano wa Sovieti ulipoivamia Afghanistan.
Alipokwenda Aghanistan, Osama alikuwa kijana sana ambaye alitaka kujijengea umaarufu, katikati ya vita vitakatifu. Osama bin Laden alikaa kwa kipindi cha takriban miaka 10 nchini Afghanistan, na kuanzisha fungamano na wanaharakati wa siasa kali za kiislamu kote duniani.
Na baada ya majeshi yaliyovunjika moyo ya Sovieti kuondoka Afghanistan mnamo mwaka 1989. Osama bin Laden alirejea nyumbani Saudi Arabia. Mwaka mmoja baadaye alijitolea kumpa msaada wa kijeshi mfalme Fahad wakati Iraq ilipoivamia nchi jirani ya Kuwait. Lakini Osama alipatwa na mshtuko mkubwa pale Mfalme Fahad alipokataa toleo lake na badala yake kuigeukia Marekani.
Osama alinyaganywa uraia wa Saudi na akarejea Afghanistan ambayo wakati huo ikitawaliwa na Wataliban ambao alikubaliana nao kuhusu tafsiri ya uislamu.
Mnamo mwaka 1998 aliwahimiza waislamu wawauwe Wamarekani mkiwemo raia popote pale watakapowapata, kukafuatiwa mashambulio kadhaa ikiwa ni pamoja na dhidi ya balozi za Marekani katika Kenya na Tanzania na manowari ya USS Cole katika mwambao wa Yemen. Halafu shambulio la September 11, 2001.
Nyumba ya ghorofa ambamo bin Laden anaaminika alikutwa na kuuawa.

Osama bin Laden aliwasifu waliofanya shambulio hilo. Rais Bush akasema atasakwa apatikane akiwa hai au mfu.
Rais Bush alikunukuliwa kusema: "Sijui kama tutampata kesho au mwezi ujao au mwaka ujao. Lakini hapana shaka tutampata tu."
Ingawa Waislamu wengi walilaani vifo vya watu katika miji ya New York na Washington, Osama bin Laden alichukuliwa na wengi kuwa ni shujaa, aliyetetea haki za Wapalestina na kupinga nguvu za Marekani.
Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama bin Laden anaaminika kuacha watoto 17.

Zaidi ya watu 600,000 wamekimbia tangu kuzuka machafuko Libya:OCHA

Libya Chakula
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema takribani watu 530,000 wameshapokea msaada wa chakula ndani ya Libya, ingawa kuna taarifa za mapigano makali yanayoendelea katika sehemu za Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa OCHA mahitaji mapya ya kibinadamu yamebainika , yakiwemo matatizo makubwa ya kiusalama kutokana na masalia ya silaha za vita. Tangu kuzuka kwa machafuko watu zaidi ya 650,000 wameondoka nchini Libya na kuanzia wiki jana mapigano yameshika kasi Kaskazini Magharibi hasa maeneo ya Zlitan, Khums, Brega, Misrata, Zawyiah na baadhi ya maeneo ya milimani ya Nafusa.
OCHA inasema ingawa msaada unawafikia waathirika, vikwazo na hasa wa kisalama vinaendelea kutia dosari operesheni za misaada na kutathimini hali halisi ya mahitaji ya kibinadamu.

Tuesday, June 28, 2011

Simba kumuuza Okwi mil. 150/-



UONGOZI wa klabu ya Simba umesema upo tayari kumuuza mshambuliaji wao, Emmanuel Okwi kwa klabu yoyote kwa kitita cha dola 100,000 za Marekani (sh. milioni 150).
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, hawaoni tatizo kumuuza Okwi, lakini lazima klabu inayomuhitaji iwe tayari kulipa kiasi hicho cha pesa.
Msimamo huo wa Simba umekuja siku chache baada ya kuwepo na taarifa kwamba, African Lyon imekuwa ikihaha kumsajili mshambuliaji huyo kutoka Uganda.
Rage alisema ameshangazwa kusikia kuwa, viongozi wa African Lyon wameshaanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo bila ya kupata ridhaa ya viongozi wa Simba, jambo alilodai ni kinyume na taratibu za usajili.
"Kwa kweli nawashangaa sana hawa African Lyon, kama wanatumwa au wana nia nzuri, waje kwetu kuomba kuzungumza na mchezaji huyo na wakikubaliana naye, watulipe dola 100,000 tuwape Okwi,"alisema Rage.
Rage alisema anahisi viongozi wa African Lyon hawafahamu vyema sheria na kanuni za usajili, hivyo amewataka wazisome na kuzielewa vyema katika kipindi hiki cha usajili.
"Sisi hatukatai kumuuza Okwi, kama wana ubavu waje na dola 100,000, kinyume na hapo haiwezekani na kama wamempa pesa zao, wajue wazi kamba wameliwa,”alisisitiza.
Kwa mujibu wa Rage, mchezaji huyo ana mkataba na Simba hadi mwaka 2012, hivyo kama kuna klabu inayotaka kumsajili, italazimika kuvunja mkataba wake.
Akizungumzia usajili wa Simba kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, Rage alisema unaendelea vizuri na kuongeza kuwa, wamepanga kutumia sh. milioni 375.
Alisema kazi ya usajili wa wachezaji wapya inafanywa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope na kusisitiza kuwa, ana imani kikosi cha timu hiyo msimu ujao kitakuwa tishio zaidi ya Yanga.

Andre Villas Boas kocha mpya wa Chelsea atangaza kuendeleza kasi yake katika klabu hiyo

Muda mfupi baada ya kuwasili Chelsea, Villas Boas alisema anataka kuendelea na kasi yake aliokuwa nayo na timu ya Porto na kushinda vikombe.
Kocha huyo mpya wa Chelsea, Andre Villas Boas alisema katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari kuwa lengo lake lilikuwa ni kushinda vikombe na hii ndiyo sababu anaelekea kujenga timu ya ushindini:
Kocha huyo alinukuliwa akisema"Hakuna shaka kwamba changamoto kubwa kwangu ni kuendelea kushinda. Mimi ni mtu mwenye kiu ya ushindi na mafaanikio natumai kuendelea hivyo. Tunataka kutengenza timu yenye nguvu. ni lazima kutafakari juu ya mafanikio ya klabu katika misimu sita iliyopita, kiwango cha kufikiwa na nini tunaweza kufanya kwa sasa na katika miaka ijayo
Mshindi wa msimu uliopita na wa kihistoria akiwa na klabu Porto (michuano, Kireno Super Cup, Kombe la Ligi na Europa), kocha huyo mwenye umri wa miaka 33, kasi yake imeongezeka mithili ya mwanga wa juwa. Mwaka (2009-2010): Académica Coimbra, 2010-2011: FC Porto, 2011-2012: Chelsea). Kama wasemavyo wataalamu sidhani kama kupanda kwa kasi kwa sifa ya kocha huyo hakuwezi kusitisha mfaanikio yake.
 Baada ya timu hiyo ya Chelsea kufanya kufuru ya usajili wa makocha, kocha huyo mpya sasa anafkiri kumsajili Mshambuliaji wa Inter milan Samuel Etoo Fils kwa kitita cha Yuro milioni 30 na mshabara wa milioni 10. samauel Etoo Fils ikiwa makubaliano yatafikia kikomo, ataungana kwenye mstari wa ushambuliaji na Fernando Torres. Tayari Samuel Etoo ameshaonyesha nia yake ya kumalizia msimu wake katika ligi ya Uingereza
Ujio wa Samuel Etoo Chelsea unaashiria kuondoka kwa Didier Drogba au Nicolas Anelka ambapo timu ya Inter milan imependekeza euro Milioni 10 kwa Nicolas Anelka

Monday, June 27, 2011

Aunty Ezekiel the most sexiest gal in Tz...........................!

Aunt Ezekiel 
Kufuatia mvutano ulioibuka nchini juu ya msichana namba one kwa mvuto wa mahaba blog yako hii inatiririka na full habari kutoka chini ya kapeti. Taarifa za kina ambazo zinafuatia kura za wadau kwa week mbili mfululizo uchunguzi ulioendeshwa na moja ya kampuni kubwa kabisa ya burudani nchini yenye makao yake makuu pande za city centre posta umeanika wazi kuwa star wa filamu ambaye anatajwa kuwa ndo laaziz wa moyo wa nguli Steven Kanumba bibiye machachari Aunty Ezekiel ni moto wa kuotea mbali kwa jinsi alivyoumbika kuanzia figure, reception na mapozi ya aina yake vitu ambavyo kwa ujumla wake vinatajwa kuwatoa udenda madume wengi kila pembe ya bongo ambao hawaachi kumzonga zonga mrembo huyo kila uchao.

Aunt ezekiel atia kinyaa kwa kuvaa nusu uchi kigali-rwanda

 

Yule muigizaji wa kimataifa wa nchini tanzania ambae majuzi akiongozana na baadhi ya waigizaji wa dar ametia kinyaa uwanja wa kigali na kufikia kila mtu kuanza kutukana kinyarwanda
aikuwa rahisi kusikia mnyarwanda akisema aiseee watanzania ni maraya sana aisee embu kumwona kale kabint kweri kamepanda ndege hata siamini kamewezaje kupita uko....

Huku wengine wakisema wanawake wa kitanzania awana aibu wara awajiheshimu wengi waliishia kumfwata na kuangalia mapaja yake huku wakati akikaa sehemu za nguo za ndani kutuna kama if kuna mdudu anataka kutoka.....Kwa wale watanzania mkienda kwa watu embu jiheshimuni jamani
hapa mnaona wanwake wote ndio wanatukanwa sio huyuhuyu tu mnaonekana wote baraya ba kibongo

 

Bob Junior Ndani ya Bifu na Wema Sepetu

Bob Junior Ndani ya Bifu na Wema Sepetu Ni kama vile Bob 'Rais wa Masharubaro' Junior ameamua kuingia kwenye 'mapambano' na kila anayekutana naye. Kutoka kwenye blogu ya Bongo Star Link, Dj Choka anatufahamisha ifuatavyo;
Habari nilizozipata mida hii kutoka kwa Rais wa Masharobaro Bob Junior ni kwamba kesho asubuhi ameitwa kituo cha Police pale Ostabey yeye na Wema Sepetu. Kisa hicho ni kwamba leo mchana Wema alienda kituoni pale kwenda kumchukulia Bob Junior RB yake hatimaye Wema akaingizwa yeye ndani kituoni hapo na kuambiwa kuwa alikuwa anatafutwa na Police.

Kisa cha Bob Junior kumpeleka Wema police ni matusi ambayo ametukanwa na Wema na yeye akawa na ushahidi wa kumrekodi na kuipeleka sauti hiyo ya matusi police na kumchukulia RB.

Sunday, June 26, 2011

Ni kweli ustaa Tanzania haupatikani bila skendo?

 

Vichwa vya habari kwenye magazeti vilivyojaa skendo chafu za wasanii wa filamu wa Tanzania

SEKTA ya filamu katika nchi yoyote ile ni sekta yenye nguvu sana, ikizingatiwa kuwa ina uwezo wa kuchangia kwa kiasi kikubwa mno katika uchumi wowote. Sekta hii ina uwezo mkubwa sana wa kuwa kichocheo cha ukuaji wa maendeleo ya haraka na ya kweli ya taifa ya nchi yoyote kwa kuzingatia utamaduni na saikolojia kwa maendeleo halisi na endelevu.

Ingawa sekta ya filamu ni moja tu kati ya sekta nyingi ndani ya tasnia ya burudani inayosimamia ubunifu, lakini filamu zinaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana wa kushawishi ama kutumika kwa ajili ya kuelimisha au kupotosha mambo katika jamii yoyote.

Tasnia ya burudani na ubunifu inajumuisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya filamu na maigizo, muziki, ulimbwende, mavazi na sanaa zingine za kiufundi, hata hivyo sekta ya filamu ni aina ya sekta inayojipambanua katika kusimamia juhudi za kitaaluma kuhusu uzalishaji na uuzaji wa mawazo katika aina mahsusi ya picha halisi itumikayo kuunganisha mahitaji, matumaini na matarajio ya jamii.

Sinema zinakusudiwa katika kuwapa watu fursa ya kusimulia hadithi zao, na kuwaacha na uhuru wa mawazo kutokana na kuingiliwa na mambo ya kigeni. Kwa hali hii watayarishaji na wasanii wa sinema wa Kitanzania wanapaswa kuishi katika maadili yasiyokinzana na maisha ya jamii na utamaduni.

Kila nikiangalia kwa makini hali halisi ya sekta ya filamu hapa nchini, sioni kama kutakuwa na '
future' yoyote katika tasnia hii endapo mambo yataendelea kuachwa yaende ovyo ovyo kama ilivyo sasa. Ikumbukwe kuwa sekta ya filamu ya Tanzania ni sawa na kinda la ndege linalotegemea mzazi alilishe chakula. Ni kama mtoto anayeanza kutembea, ambaye kila aina ya dosari ni mambo ya kawaida yanayotarajiwa kutokea.

Hata hivyo, katika mazingira ya upatikanaji wa miundombinu ya kimasoko katika kulikuza soko la filamu nchini na kimataifa, Wasanii wa Kitanzania wanastahili kuwa na sifa nzuri katika kuhakikisha kuwa tasnia hii inaaminiwa na watu wote wakiwemo wawekezaji.

Nikiwa mwanaharakati na mdau muhimu sana katika sekta hii, kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikijionea vituko hivi na vile kutoka kwa wasanii wetu hasa wanaojiita mastaa, ambao wamediriki kusema kuwa huwezi kuwa maarufu kama huna skendo. Jambo hili linawafanya wasanii wengi katika tasnia hii wasiopenda kujihusisha na kashfa yoyote kukabiliwa na changamoto nyingi za kila siku.

Baadhi ya matatizo haya ni ya asili ya kimataifa, wakati mengine ni ya kipekee kwa jamii mbalimbali.

Miongoni mwa mambo ambayo yamezoeleka sana katika jamii yetu hivi sasa kiasi cha kuzifanya akili zetu kuamini kuwa ni mambo ya kawaida kwa msanii yeyote mwenye umaarufu ni pamoja na kusoma habari zenye kuhusiana na skendo mbalimbali za wasanii wetu. Wasomaji wa magazeti pendwa ambayo wengine hupenda kuyaita ya udaku watakuwa ni mashahidi wa jambo hili, kwani ukifuatilia kwenye magazeti hayo wiki nzima utabaini hili kwa urahisi sana.

Hali hii mara kwa mara imekuwa ikizua malalamiko kwa baadhi ya wasanii wenyewe ambao wamekuwa wakiandikwa kwa mabaya yao wanayoyatenda, na pia hata jamii ambayo imekuwa ikiwafuatilia na kufuatilia habari zao pia. Jambo hili ukilitazama kijuujuu unaweza kuyalaumu magazeti hayo na waandishi wanaowaandika vibaya wasanii kwa kudhani kuwa wanavuka mipaka na kuingilia mambo binafsi, lakini kumbe kuna jambo nyuma ya pazia.

Wasanii karibu wote wa nchi hii, maarufu na hata wasiokuwa maarufu nawafahamu vizuri sana, nimewahi kufanya nao kazi na wengine nimewasaidia kuingia kwenye fani hii ya sanaa ya filamu na maigizo. Ukweli ni kwamba walio wengi huwa wanajipeleka wenyewe kwa waandishi ili waandikwe vibaya kwa dhumuni la 'kutoka kisanii', ndiyo maana wengi wao hata wakiandikwa vipi huwasikii kulalamika au kuchukua hatua zozote. Si hivyo tu, hata pale wasanii hawa wanapohisi kuwa umaarufu wao umeanza kuchuja huwatafuta waandishi wa magazeti hayo ili kuosha nyota!

Wengi wa wanaojiita mastaa wa Bongo waliopata umaarufu kupitia skendo za magazetini huwa hawaijui thamani ya ustaa wao hata pale wanapokuwa tayari maarufu. Hii ni kutokana na skendo zao za ngono mfululizo tunazozisoma magazetini ambazo kwa kweli ni ujinga mtupu!

Inashangaza kuona mtu akitokea kwenye filamu moja au mbili tu, tena kwa kushirikishwa kwenye sehemu ndogo ya sinema hiyo, ataanza kujiita staa na kujiingiza kwenye kujitafutia skendo kwenye magazeti ili asomwe. Ndiyo maana utakuta kila kukicha kunaibuka skendo za aibu kibao!

Mfano ni binti mmoja mwenye asili kama Mmanga ambaye kwa sasa anavuma sana kwa skendo za usagaji kwenye magazeti, ni mwaka jana tu alikuwa akinipigia magoti nimuunganishe aweze kuigiza filamu na wasanii maarufu, siku moja akabahatika kushirikishwa kwenye filamu na mmoja wa wasanii maarufu hapa nchini kwa kupewa sehemu ndogo tu ya kuigiza, eti hivi sasa naye anatembea mabega juu huku akitamba kwenye magazeti kwa kashfa za usagaji, kufumwa na midume usiku na nyingine kibao!

Pia kuna wakati niliwahi kufuatwa na msanii mmoja wa kike (jina nalihifadhi) ambaye wakati huo hakuwa na umaarufu kama alionao sasa, aliyetaka iandikwe skendo yake ya kugombewa na mabwana wawili ambao walikuwa viongozi ndani ya kundi la filamu alilokuwa akifanyia mazoezi. Nilimwelekeza mahali pa kupeleka habari zake huku nikimwambia ukweli kuwa mimi si mwandishi wa kufanya promosheni za aina hiyo, bali mimi ni mchambuzi ambaye naitazama sekta nzima ya filamu, mazuri na changamoto zake na kuihabarisha jamii pasipo kujishughulisha na mambo binafsi ya mtu.

Mifano hai ya wasanii wanaoamini kuwa huwezi kuwa maarufu bila kuibua kashfa iko mingi kiasi kwamba nikianza kuwataja nitajaza kurasa zote za gazeti hili na nisiimalize, japo siyo wasanii wote wanaopenda kuandikwa vibaya kwenye magazeti. Wapo baadhi ya wasanii waliokuwa maarufu sana wakati fulani lakini hawakuwahi kuandikwa vibaya kwenye magazeti, na hawakuwahi kuwafuata waandishi ili wawaandike hata kwa jambo zuri kwani waliamini kuwa kazi zao ndizo zilizokuwa zikiwafanya wajulikane.

Sikatai, wapo baadhi ya wasanii hasa wale wanaolalamika baada ya kuandikwa vibaya kwenye magazeti huwa hawapendi kufuatiliwa katika masuala yao binafsi na kuyaweka kwenye vyombo vya habari, lakini mambo ya kuibuka skendo mbaya kila kukicha yanawafanya hata wasanii wenye maadili mema kuogopa kujitambulisha kwa watu kuwa ni wasanii.

Najua kuwa suala la mapenzi halina mipaka na lingeweza kutokea wakati wowote na kwa mtu yeyote hata kwangu mimi ninayeandika, na kama linatokea kwa wasanii wawili watatu hakuna ubaya wowote, lakini hali ilivyo sasa imekithiri kiasi cha kutia kinyaa.

Utakuta msanii wa kike anajilengesha kwa 'pedeshee' fulani halafu akikubaliwa anamfuata mwandishi wa habari na kumwambia aibue skendo kuhusu uhusiano wake na mtu huyo, tena atamtafutia hata picha. Akishaandikwa gazetini atajifanya kulalamika kuwa waandishi wanamfuatilia maisha yake kwa kuwa yeye ni staa!

Iliwahi kutokea kwa msanii mmoja wa kike aliyetamba sana kwenye magazeti enzi hizo kwa kashfa mbalimbali na baadaye akaingia kwenye ugomvi na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki maarufu wa bongofleva aliyeamua kumuimba vibaya. Msanii huyu wa kike aliyependa sana kuandikwa vibaya lakini baada ya kuamini kuwa ameshapata ustaa alioutaka hakutaka tena kuandikwa kwa mabaya aliyoyafanya, kiasi cha kujisingizia kunywa sumu.

Pia utakuta msanii wa kiume anaamua kutembeza urijali wake kwa wacheza filamu wa kike karibia wote katika kundi lake akiwa hajali kuwa ipo siku watakuja kujuana, halafu anamfuata mwandishi ili aandike tena ikibidi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti kuwa yeye ni kiwembe!

Ule msemo kuwa “ustaa hauji bila skendo” hauna ukweli wowote, ukijiuliza sana wakati wasanii kama Bishanga, Rich Richie, Waridi, Aisha na wengineo wanavuma walitumia skendo zipi kuwafikisha hapo walipokuwa? Au wasanii kama Lumole Matovolwa (Biggie Poppa), Yusuf Mlela, Kemmi, Monalisa, Natasha na baadhi ya wasanii wa aina yao mbona wamepata umaarufu mkubwa bila kuwa na skendo?

Leo hii imekuwa ni jambo gumu sana kwa wasanii walio wengi endapo utaamua kumwita msanii ukataka kumuandika kwa mazuri yake, kwa kuwa walio wengi wanaamini kuwa mambo mazuri hayawezi kuwafanya watoke.

Babu wa Loliondo "avuliwa nguo"

Default 

"Hapa Arusha KILA HOSPITALI IMEPOKEA WATU WA MAGONJWA YA PRESHA, KISUKARI, PUMU, N.K. AMBAO WALIKWENDA LOLIONDO "KUTIBIWA" MARADHI HAYO NA BAADA YA KUPATA "NAFUU" (PSYCHOLOGICAL) KWA KAMA WIKI MBILI TU WAMEANZA KUUMWA SERIOUSLY NA KURUDIA DAWA ZAO ZA HOSPITALI TENA.

Pili, mimi nikiwa mfanyakazi wa maabara ya hospitali ya MT Meru, sijaona hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepata "seroconversion" yaani kurudi "seronegative from serpositive status". Kinachosikitisha ni kuwa kuna watu hawataki kabisa kusikia yanayosemwa na madaktari na wafanyakazi wa hospitali mbalimbali hapa Arusha ambao kila siku tuna-deal na watu wanaozidiwa baada ya kwenda Loliondo.


Mbaya zaidi kuna magazeti, tv na redio hayataki kabisa kusikia ukweli wa majanga yaliyowafika watu waliokwenda huko. Ajabu pia ni kuwa kuna watu ambao ukitaka kuwaeleza ukweli wanakuona wewe ni mpagani usiyemwamini Mungu. Naomba waandishi wa habari wawe proactive katika kutafuta ukweli na si kutegemea mass hysteria iliyowakumba maelfu ya watu wanaotafuta miujiza kwa nguvu."

Source: MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo: Kama Haya Ni Ya Kweli